Tarehe 25 Januari 2024, Mhe. Ali Jabir Mwadini, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa ambae pia ni Mwakilishi wa Kudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UN Tourism) lenye makao makuu yake jijini Madrid, Uhispania aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Katibu Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Zurab Pololikashvili kwenye makao makuu ya Shirika hilo.
Baada ya tukio hilo, Viongozi hao walijadili mikakati ya kukuza utalii nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuongeza mbinu za kutangaza vivutio vya Tanzania na kuimarisha huduma za usafiri kutoka miji inayotoa watalii wengi kwenda Tanzania.