Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake jijini Paris, kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na mashirika makubwa ya ndege yanayofanya safari zao ndani na nje ya bara la Ulaya.  Mashirika hayo ni Air  Europa, Iberia, Plusultra na W2M yote ya Uhispania. Aidha, alikutana na Bw. Rosa, mwenye kampuni inayoratibu ndege maalum (charter flights) za kitalii kutoka Lisbon. Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kujadili mipango ya kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya miji mikubwa ya Uhispania na Ureno na miji ya Tanzania ili kurahisisha usafiri na kuimarisha utalii.