Mheshimiwa Balozi Ali Mwadini amekabidhi nakala za Hati za Utambulisho kwa Bi. Maria SEBASTIAN DE LA PEÑA, Mkurugenzi Mkuu wa Itifaki kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Uhispania.
Aidha, kwa nyakati tofauti Balozi Mwadini amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika; na Mkurugenzi Mkuu wa Siasa za Kimataifa na Usalama katika Wizara hiyo. Katika mazungumzo, viongozi hao wamekubaliana kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Uhispania katika masuala ya diplomasia, uwekezaji, biashara, nishati safi na utalii.