Balozi Mwadin  alipokutana na Mhe. David Doyle, Balozi wa Visiwa vya St. Kitts and Nevis (SKN) nchini Ufaransa na pia Mwakilishi wa Kudumu wa visiwa hivyo kwenye UNESCO.

Kwa pamoja walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano hususan utayari wa Tanzania kupitia Chuo Kikuu Huria (OUT) kushirikiana na visiwa hivyo katika kutoa mafunzo kwa walimu wa SKN kwa mpango  wa Mafunzo ya Mtandao na Masafa (Online and Distance Learning - ODL)