Balozi Mwadini amekutana na Mhe. Ronan Dantec, ambaye ni  Mwenyekiti wa Kikundi cha Urafiki cha Maseneta wa Ufaransa na Nchi za Bahari ya Hindi ikiwemo Tanzania tarehe 6 Februari 2024.

Katika mazungumzo yao, wamekubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa kwa kutumia Diplomasia ya Kibunge (Parliamentary Diplomacy).

Aidha, wamejadiliana kuhusu  namna ambavyo ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa unaweza kuimarishwa kupitia sekta nyingine mbalimbali.