Balozi Ali Mwadini amekutana na Wanadiaspora wa Tanzania waishio Ufaransa ambapo amewapongeza kwa ushirikiano na mshikamano wao. Pia amewaasa kuishi kwa kufuata sheria za nchi mwenyeji ili kutoharibu sifa ya Tanzania.

Vilevile Balozi Ali Mwadini amewahimiza Wanadiaspora kuendelea kuweka nyumbani kupitia fursa mbalimbali zilizopo.  Ametaarifu pia kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea na jitihada zake za kuboresha utoaji huduma mbalimbali kwa Wanadiaspora.