Balozi Mwadini awawasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Mhe. Nasser Bourita, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika na Raia wa Morocco waishio Nje ya Nchi. Mhe. Balozi Mwadini na Mhe. Bourita walijadiliana pia kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Falme ya Morocco katika sekta mbalimbali.