Pamoja na mambo mengine lengo la mkutano  huo ilikuwa kuelezea fursa za masoko nchini Ufaransa kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Mkutano huu ulitanguliwa na ziara ya siku mbili(2), tarehe 17 na 18 Aprili,2018, jumla ya wafanyabiashara 35 kutoka Ufaransa ambao walikuja nchini kuangalia fursa za uwekezaji. 

Akiongea katika Mkutano huo Mhe. Balozi Shelukindo alisema, kuna fursa nyingi sana nchini Ufaransa hasa katika mazao ya vyakula, mbogaboga na matunda hivyo Serikali iko tayari kusaidia pale msaada wa jinsi ya kufikia hayo masoko utakapohitajika. Naye Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Clavier ametoa rai kwa wafanyabiashara kuutumia Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini kwa ajili ya kupata taarifa jinsi ya kulifikia soko la Ufaransa.

Kwa mujibu wa Balozi Shelukindo mazao yanayohitajika zaidi nchini humo ni asali, mbogamboga na matunda, viungo, nyanya, kahawa, samaki, chai na cacao.

  • Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier akiongea na vyombo vya habari katika mkutano huo.
  • Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano huo
  • Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika Mkutano
  • Mkurugenzi wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka, akifafanua jambo katika mkutano huo
  • Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvatory Mbilinyi akiongea katika Mkutano huo.
  • Bi. Mona Mahecha, Afisa Mambo ya Nje(wa kwanza) na wajumbe wengine wakifuatilia Mkutano
  • Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi Mindi Kasiga ambaye alikuwa Mshehereshaji wa Mkutano huo akiongea jambo.
  • Mkutano ukiendelea
  • Balozi Clavier akiongea na vyombo vya habari baada ya Mkutano, pembeni yake ni Balozi Shelukindo akisikiliza.
  • Balozi Shelukindo na Balozi Clavier akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara baada ya Mkutano.