Mhe. Samwel W. Shelukindo, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye UNESCO, akiwasilisha hotuba ya nchi katika Mkutano wa 215 wa Bodi Tendaji ya Shirika hilo tarehe 11 Oktoba 2022, jijini Paris. Mh Balozi ameipongeza UNESCO kwa utekelezaji mzuri wa mipango na bajeti yake ya mwaka 2022-2023 ktk sekta za elimu, sayansi na utamaduni. Pia, amethibitisha utayari wa Tanzania  katika kushirikiana na UNESCO kwenye mkakati wa mwaka 2022-29 unaochochea maendeleo ya Afrika (Priority Africa). Aidha ameipongeza @GlamiTanzania kwa kutwaa tuzo maalumu ya UNESCO  inayotolewa kwa minajili ya kutambua mchango wa taasisi zilizofanya vizuri zaidi katika kuimarisha utoaji wa elimu kwa wanawake na wasichana. Tuzo hizo zimetolewa  tarehe 11.10.2022 jijini Paris Ufaransa.Kwa mwaka huu, tuzo hiyo inayofadhiliwa na China, imetolewa kwa taasisi mbili pekee, yaani @GlamiTanzania na taasisi nyingine ya "Room to Read" kutoka Cambodia, kati ya taasisi 75 zilizowania tuzo hiyo kutoka nchi 48 duniani kote.