Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bw. Yakubu akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa,  Mhe. Samwel Shelukindo, tuzo kwa kutambua mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili.

Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ulifanikisha kupitishwa kwa azimio la UNESCO la kuitambua siku ya tarehe 7 Julai kila mwaka kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani.