Mhe. Samwel W. Shelukindo, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwenye UNESCO, akishiriki katika mjadala kwa niaba ya Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb.), Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Mkutano wa UNESCO kuhusu uboreshaji wa Sera za Utamaduni na Maendeleo Endelevu (MONDIACULT) unaoendelea jijini Mexico, 28 - 30 Septemba 2022.