Tarehe 20 Agosti,2022, Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana, aliongoza ujumbe wa Wizara kwenye kikao baina ya Kitengo hicho na viongozi wa Diaspora wa Chama Cha Watanzania Waishio Ufaransa (CCWU) kilichofanyika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Paris. Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo, alishiriki kikao hicho. Viongozi wa CCWU walioshiriki ni Makamu Mwenyekiti, Bw. Julius Myombo; Katibu Mkuu  Bw. Collins Mtita na Katibu Msaidizi, Bw. Deogratias Amos.