Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Mb., yupo Madrid, Uhispania ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii wa nchi hiyo, Bi. Xiana Mendez. , ambapo Uhispania imeonesha nia ya kushiriki kagika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa kutoa mkopo, dhamana ya mikopo na Bima kwa Kampuni za nchi hiyo zitakazojenga reli hiyo kuanzia Makutopora hadi Mwanza na Kipande cha kuanzia Tabora-Kigoma hadi Malagarasi, kutokana na umuhimu wa ì huo kwa maendeleo ya nchi.