Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Bw. Khamis Omar akitiliana saini na Bw. Rui de Sa Pessoa Mkataba wa kumteua Bw. Rui de Sa Pessoa kuwa Konseli wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Lisbon, Ureno.

Utiaji saini huo umefanyika leo tarehe 29 Mei 2023 katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania, Paris.

Kufuatia utiaji saini mkataba huo, Bw. Omar na Bw. Sa Pessoa walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa watu wa pande mbili hizi, ikiwemo kutembeleana kwa njia ya utalii, michezo na utamaduni, na kutangaza fursa nyingi za uwekezaji na biashara zilizoko katika nchi hizo.