Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb.), Waziri wa Maliasili na Utalii ameongoza Mkutano wa 25 wa Baraza Kuu la Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) unaloendelea jijini Samarkand, Uzbekistan. Katika Mkutano huo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatumikia nafasi ya Makamu wa Rais wa Baraza kwa mwaka 2023-2025.