Ubalozi wa Tanzania Paris kwa kushirkiana na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar (ZCT), wamefanikisha ushiriki wa makampuni 15 ya wadau wa utalii kutoka Bara na Zanzibar kwenye maonesho makubwa zaidi ya utalii nchini Ufaransa ya International French Travel Market Exhibition (IFTM Top Resa 2024). Maonesho hayo yalianza tarehe 17 na kumalizika tarehe 19 Septemba 2024, katika ukumbi wa Porte de Versaille, Paris. Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum (MBM), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango Zanzibar alishirki maonesho hayo siku ya tarehe 19 Septemba 2024 na kushiriki pia mikutano mbalimbali ya pembezoni.