Ubalozi kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Chama Cha Watanzania Ufaransa (CCWU) unapenda kuwataarifu Wanadiaspora wa Kitanzania waishio kwenye eneo la Uwakilishi kuwa unatarajia kuendesha mafunzo mafupi kwa Wanadiaspora wakufunzi na wanaotarajia kuwa wakufunzi wa lugha ya Kiswahili kwa wageni.