Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii (FITUR), yanayoendelea mjini Madrid limevuta makampuni mengi ya utalii pamoja na watu mmoja mmoja wanaotafuta nchi za kutembelea. Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambao unaiwakilisha pia Tanzania nchini Uhispania, unaratibu ushiriki wa Wadau wa utalii kutoka Tanzania katika maonesho hayo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Ngorongoro. Maonesho hayo yalianza tarehe 24 Januari 2024, yanahitimishwa tarehe 28 Januari 2024