Tanzania imeshiriki kikamilifu maonyesho ya Utalii nchini Ufaransa kwa mafanikio makubwa. Ushiriki wa Tanzania  kwa mwaka huu umekuwa mkubwa kutokana na mkazo uliosisitizwa na Serikali katika kukuza sekta ya Utalii. Inategemewa kwamba watalii kutoka Ufaransa kuja Tanzania wataendelea kuongezeka. Idadi ya watalii kutoka Ufaransa imeongezeka kutoka 24,000 mwaka 2016 mpaka 41,000 mwaka 2018.