Timu ya Serengeti Girls (U-17) imetwaa kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nchi za Afrika Kaskazini leo kufuatia kutoka sare ya 0-0 na wenyeji Tunisia. Timu hiyo iliyong’ara sana na kuwa gumzo mjini Tunis imeibuka ya kwanza baada ya kuwa na idadi kubwa ya magoli ya kufunga ikifuatiwa na Tunisia.