Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wasichana chini ya miaka 17 (U17), ipo mjini Tunis, Tunisia kushiriki Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nchi za Afrika Kaskazini (UNAF). Katika michuano iliyoanza tarehe 03/09/2024, katika mechi ya ufunguzi, Tanzania iliiachapa Misri 4-1 na Tunisia kuifunga Morocco 2-0. Timu nne zinashiriki michuano hiyo ambapo tarehe 05/09/2024, Tanzania inacheza na Morocco. Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa, unaowakilisha pia nchini Tunisia unashirikiana na Uongozi wa timu hiyo ili kuhakikisha inafanya vizuri katika mashindano hayo.