Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye UNESCO umeungana na nchi zingine duniani kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Lugha Mama. Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Februari katika Makao Makuu ya UNESCO jijini Paris, Ufaransa.