Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa amekutana na kundi la wanafunzi wa shule ya St. Mary Goreti Secondary School, Moshi ambao wametembelea Ubalozi ili kujifunza shughuli za Kibalozi na masuala mengineyo ya Uwakilishi, ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kimafunzo katika baadhi ya nchi za Ulaya. Msafara wa wanafunzi hao unaongozwa na Mwalimu Mkuu wa shule, Sr. Clementina M. Kachweka.