Tarehe 16 Mei 2023, Bw. Khamis M. Omar, Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao pia ni Uwakilishi wa Kudumu kwenye UNESCO amewasilisha hotuba ya Tanzania kwenye Kikao cha 216 cha Bodi Tendaji ya UNESCO kinachoendelea kwenye Makao Makuu ya UNESCO, jijini Paris. Kwenye maelezo yake, Tanzania imesisitiza UNESCO kuongeza kasi ya utekezaji wa programu zake kuhusu elimu, sayansi, utamaduni na mawasiliano katika nchi za Afrika.