Ubalozi Washiriki Tamasha la Kimataifa la Vyakula (Village
international de gastronomie) linalofanyika mjini Paris tarehe 1 hadi
4 Septemba, 2022.
Katika tamasha hilo, Ubalozi umewashirikisha pia Wanadiaspora wa
Tanzania waishio Paris ambao walipika vyakula vya asili ya Tanzania
pamoja kuonyesha bidhaa mbalimbali za vyakula na vinywaji kutoka
Tanzania.
Tamasha hilo hufanyika kila mwaka na limekuwa moja ya fursa za
kuitangaza Tanzania siyo tu kwa vyakula na vinywaji bali pia fursa
hiyo hutumika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.